Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kutoa ruzuku ya mbolea kwa mazao yote

Mbolea 1 Serikali kutoa ruzuku ya mbolea kwa mazao yote

Tue, 12 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa Serikali itatoa ruzuku ya mbolea kwa mazao yote ya kilimo ili kuepuka makosa yaliyokuwepo hapo awali.

Bashe ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 12, 2022 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Namtumbo (CCM), Vita Kawawa.

Katika swali la nyongeza, Kawawa amehoji kama Serikali inaweza kuweka mpango wa kutoa ruzuku kwa mazao ya mpunga na mahindi kutokana na ongezeko kubwa la bei ya mbolea.

Katika swali la nyongeza Kawawa amesema kutokana na ongezeko kubwa la bei ya mbolea, Serikali inaweza kuweka mpango wa kutoa ruzuku kwa mazao ya mpunga na mahindi.

Amehoji kwa kuwa wakulima walilima kwa gharama kubwa katika msimu uliopita, Serikali iko tayari kutangaza mapema ili wakulima waweze kupata bei katika soko la mahindi katika msimu huu.

Akijibu maswali hayo, Bashe amesema baada ya Julai Mosi mwaka huu watakaa na Wizara ya Fedha na Mpango kwa ajili ya kutengeneza muundo wa namna watatoa ruzuku kwenye mbolea. 

Advertisement Kuhusu bei elekezi ya mazao, Bashe amesema baada ya kupitisha bajeti ya kilimo NFRA itatoa bei ambayo itakayonunulia mazao.

Katika swali lake la msingi, Kawawa alihoji Serikali inachukua hatua gani kudhibiti kuongezeka kwa bei ya mbolea nchini hasa mkoani Ruvuma?

Akijibu swali hilo, Bashe alisema Serikali imeweka utaratibu wa kudhibiti upandishaji holela wa bei za mbolea unaoweza kufanywa na wafanyabiashara bila kuzingatia gharama halisi za uingizaji wa mbolea nchini.

“Utaratibu huo unahusisha Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kwa kushirikiana na mikoa kufanya tathmini ya gharama halisi ya bei ya mbolea kwa mkulima na kutoa bei elekezi,”amesema.

Amesema Machi 2022 Serikali kupitia TFRA imetoa bei elekezi za mbolea za DAP, UREA, CAN na SA kwa mikoa mbalimbali nchini ikiwamo Mkoa wa Ruvuma.

Amesema pia katika kuondokana na utegemezi wa uagizaji wa mbolea nje ya nchi, Serikali inaendelela kuvutia uwekaji wa viwanda vya mbolea hapa nchini ili kupunguza gharama za mbolea kwa mkulima.

Amesema baadhi ya wawekezaji waliojitokeza ni kampuni Itracom inayojenga kiwanda cha mbolea jijini Dodoma chenye uwezo wa kuzalisha tani 600,000 na Kiwanda cha Minjingu kuendelea na kuongeza uzalishaji kutoka uwezo wa tani 100,000 za sasa hadi kufikia tani 500,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live