Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kutoa hekari mbili kwa wakulima wa ufuta

Ufuta Pc Data Serikali kutoa hekari mbili kwa wakulima wa ufuta

Tue, 12 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Hashim Komba kupitia mahojiano yake maalum na AyoTV amesema Wilaya yake imekuja na mkakati wa kuongeza uzalishaji wa ufuta ambapo wanagawa hekari mbili za ardhi bure kwa Mtu yoyote anayetaka kulima ufuta Nachingwea.

"Tumekuja na mkakati maalumu wa kuongeza zao la ufuta ukija kwetu tunakupatia ardhi hekari mbili bure, mbegu zinazotosha kupanda shamba la hekari mbili, dawa za kuulia magugu bure na tunakupatia Mtaalamu wa Kilimo atakutembelea na kukushauri”

"Ukihitaji ardhi unafika Halmashauri ya Nachingwea unakwenda idara ya kilimo unajiorodhesha halafu tunakutajia vijiji vyote vinavyostawi zao la ufuta unaanza uzalishaji lakini tu sharti lake ni kwamba ukivuna uuzie ufuta wako Nachingwea ili tupate mapato kwakuwa Halmashauri inachukua ushuru kwenye kilo moja inayozalishwa ndani ya Wilaya yetu”

"Kwa shamba la hekari mbili unaweza kupata hadi Kilo 500 sasa unaweza kupiga hesabu hapo Kilo 500 kwa Tsh.3000 kwa kila kilo moja, unakuwa umejipatia fedha yako ya kutosha"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live