Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kutoa fursa kwa vijana sekta ya madini

MAVUNDEEEEEE Serikali kutoa fursa kwa vijana sekta ya madini

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia wizara ya Madini imeanzisha programu ya 'Mining for Better Tommorrow' (MBT) itakayowawezesha vijana kushirikishwa katika sekta ya madini kwa kujengewa uwezo, kupatiwa mitaji, vifaa na mashine ili wachimbe madini kwa uhakika bila kupoteza mitaji.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Anthony Mavunde katika kongamano la Mpango wa Ushirikishwaji Wananchi kwenye sekta ya Madini lililofanyika kwenye viwanja vya EPZ mkoani Geita, kunakofanyika maonesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini.

Akielezea kuhusu programu ya MBT, Mavunde amesema hivi sasa nguvu kazi kubwa ipo kwa vijana hivyo ni vema vijana wengi wa kitanzania wakashiriki katika sekta hiyo kupitia programu ya MBT ambayo itasimamiwa na Serikali.

Waziri Mavunde amefafanua kuwa MBT itawajengea uwezo vijana kwa kuwapatia mitaji na kuwaunganisha katika Taasisi za fedha, kuwapatia wataalam waliopo katika sekta ili wapate ushauri elekezi katika hatua za utafutaji , uchimbaji, uchenjuaji na uthaminishaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live