Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kutathimini meli ya Mtwara- Comoro

Meli Mtwara Serikali kutathimini meli ya Mtwara- Comoro

Fri, 5 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema imetenga fedha kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu (feasibility study) katika bahari ya Hindi kwa lengo la kujiridhisha na kiwango cha mahitaji ya usafiri wa meli kwa wananchi wa mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi na nchi jirani ikiwa ni pamoja na Visiwa vya Comoro.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema Upembuzi huo utasaidia Serikali kuamua aina ya Meli itakayojengwa kulingana na hitaji la wananchi na soko kwa ujumla.

“Serikali inatambua umuhimu wa mawasiliano baina yake na mataifa jirani hasa nchi ya Comoro. Serikali kupitia Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) imetenga fedha,” Naibu Waziri amesema wakati akijibu swali la Mbunge wa Newala Vijijini, Salum Mtanda.

Mbunge huyo alihoji ni lini Serikali itajenga Meli katika Bandari ya Mtwara itakayorahisisha mawasiliano na nchi ya Comoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live