Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar

Bandari Tanga Tangaaa Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“ Kuhusu uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeendelea kutekeleza kazi mbalimbali ambapo uchimbaji wa kina umefikia mita 15.5 na upanuzi wa lango la kuingia meli ambalo lina una upana wa mita 200. Kwa sasa, Bandari ina uwezo wa kupokea meli kubwa zenye urefu wa mita 305. Aidha, upembuzi yakinifu wa kuboresha Gati Na. 8 – 11 na ujenzi wa Gati Na. 12 - 15 bado unaendelea. Vilevile, mkataba wa kuendeleza miundombinu ya kupokelea mafuta (Single Receiving Terminal - SRT) unaohusisha ujenzi wa matenki 15 ya mafuta (tank farms) pamoja na miundombinu yake, yenye uwezo wa kuhifadhi kiasi cha mita za ujazo 420,000 umesainiwa tarehe 26 Februari, 2024 na maandalizi ya kuanza ujenzi yanaendelea”

“Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imeendelea kushirikisha sekta binafsi katika uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam kwa baadhi ya maeneo ya bandari kwa kuingia ubia na Kampuni Binafsi katika kuendeleza na kuendesha shughuli za bandari kuanzia Gati Na. 4 hadi 7. Kwa sasa hatua mbalimbali zikiwamo za makabidhiano na ‘mobilization’ zinaendelea ili kuruhusu utekelezaji rasmi kuanza.

Aidha, Serikali inaendelea na taratibu za kumpata Mwekezaji mwingine atakayekuwa na jukumu la kufanya shughuli za uendeshaji kuanzia Gati Namba 8 hadi 11 lengo ni kuongeza tija katika utendaji wa bandari”- Prof. Mbarawa.

Waziri Wa Uchukuzi. Prof. Makame Mbarawa akiwasilisha bungeni Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2024/25 leo Jumatatu Mei 06, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live