Menu ›
Biashara
Thu, 11 Feb 2021
Chanzo: habarileo.co.tz
Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda amesema ifikapo mwaka 2022 Serikali itasitisha utoaji wa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi kwa makampuni ambayo ndio wazalishaji wa ndani wa bidhaa hiyo.
Akizungumzia changamoto ya bidhaa hiyo leo, Prof Mkenda amesema upungufu wa bidhaa hiyo nchini hautokani na uhaba wa miwa bali unasababishwa na makampuni kushindwa kuongeza uchakataji wa miwa kutoka kwa wakulima.
“Baada ya mwaka huu Serikali haitotoa vibali kwa wawekezaji waliopewa viwanda vya sukari kuagiza sukari nje na badala yake kazi hiyo itafanywa na Bodi ya Sukari Tanzania” amesema Mkenda.
Chanzo: habarileo.co.tz