Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kusitisha utoaji wa vibali vya sukari kutoka nje.

Waziri Mkenda Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema ifikapo Mwaka 2022 itasitisha utoaji wa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi kwa makampuni ambayo ndio wazalishaji wa ndani wa bidhaa hiyo.

Upungufu wa bidhaa hiyo nchini hautokani na uhaba wa miwa bali unasababishwa na makampuni kushindwa kuongeza uchakataji wa miwa kutoka kwa wakulima.

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda ameyasema eneo la Ntyuka Jijini Dodoma aliposhiriki katika kongamano la saba la wadau wa sekta ya kilimo kuhusu sera pamoja na kutathmini shughuli za kilimo nchini.

“Baada ya mwaka huu Serikali haitotoa vibali kwa wawekezaji waliopewa viwanda vya sukari kuagiza sukari nje kwani tayari watakuwa wamefikia uwezo wa kuzalisha sukari toshelevu ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa uanzishwaji wa viwanda vipya vya sukari hapa nchini”

Waziri Mkenda amesema kuwa zaidi ya Tani 350,000 za miwa ya wakulima katika Bonde la Kilombero mkoani Morogoro zinateketezwa kwa moto kutokana na kukosa soko la uhakika lakini viwanda haviongezi uwezo wa kuchakata miwa ili kuzalisha sukari ya kutosha.

Amesema kuwa zaidi ya Tani 40,000 zinaagizwa kutoka nje ya nchi jambo ambalo sio sahihi kwani viwanda vya sukari vilivyopo nchini vinapaswa kuongeza uwezo wao ili kuimarisha soko la wakulima jambo litakalopelekea nchi kutoagiza sukari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live