Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kushusha kodi baadhi ya bidhaa nchini

Kassim Majaliwa Bungeni Serikali kushusha kodi baadhi ya bidhaa nchini

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali inakusudia kupunguza kodi katika baadhi ya bidhaa ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na ongezeko la mfumuko wa bei ya vitu na huduma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliambia Bunge mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Serikali hutoa ruzuku na misamaha ya kodi kwa baadhi ya bidhaa ikilenga kurahisisha gharama za bidhaa na huduma katika jamii.

Majaliwa hakutaja aina ya bidhaa zitakazopata msamaha huo hata hivyo amesema serikali imeanzisha utaratibu wa kufuatilia na kutathimini ofisi za umma kupitia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live