Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kusamehe ushuru  wa kuagiza simu za mkononi

93f76dec624d01bebc8d638b7dfdc2d5.jpeg Serikali kusamehe ushuru  wa kuagiza simu za mkononi

Tue, 20 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS Salva Kiir amesema serikali itasamehe ushuru wa kuagiza bidhaa za simu za mkononi ili kuruhusu kampuni kutoa huduma bora kwa raia.

Katika hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mtandao wa dijitali juzi, Rais Kiir alisema serikali itasamehe ushuru kwa waagizaji wa vifaa vya mtandao wa simu za mkononi ili kuongeza matumizi ya dijitali nchini.

"Serikali itafanya maamuzi ikiwa ni pamoja na msamaha wa ushuru ambao utafaidisha uingizaji wa vifaa vya mtandao na zana za mawasiliano," alisema.

Rais Kiir alisema hatua hiyo itaongeza uingizwaji wa vifaa vya matumizi ya mtandao katika simu za mikononi na kuongeza matumizi ya mitandao kwa wananchi.

"Msamaha wa kodi ninayopendekeza utafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato kuhakikisha njia za msamaha wa kodi zinaambatana na taratibu," alisema.

Alizitaka kampuni za simu za mkononi kupeleka huduma za simu za mkononi kwa watu wa maeneo ya vijijini ili kuongeza idadai ya watu wanaunganishwa kwenye mitandao.

Alisema kuchelewa kuwaunganisha watu katika maeneo ya vijijini kutadhoofisha juhudi za serikali za kuunganisha watu wake na wengine ulimwenguni kupitia teknolojia ya dijitali.

Chanzo: www.habarileo.co.tz