Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuruhusu Mabasi, Masoko kufanyakazi saa 24

De131370b3cd49fd3f992e67f0a0642e.jpeg Serikali kuruhusu Mabasi, Masoko kufanyakazi saa 24

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeagiza jeshi la polisi kuharakisha tathimini ya hali ya usalama nchini ili kuruhusu masoko na mabasi kufanya kazi saa 24 siku saba za wiki.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema “ni kweli sasa usalama umeimarika” tofauti na zamani ambapo serikali ililazimika kuweka polisi katika mabasi kutokana na wimbi la uhalifu hasa utekaji mabasi nyakati za usiku.

Agizo la kuzuia mabasi yasifanye kazi usiku lilitolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu, John Malecela mwaka 1994 hata hivyo hapakuwa na sera wala sheria ya tamko hilo ambalo bado linatumika hadi leo, kwa mujibu wa Mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda (CCM).

Mbunge huyo alihoji ni kwa nini sasa serikali isiruhusu mabasi kufanya kazi usiku na mchana.

“Agizo lilitolewa kwa sababu mabasi yalikuwa yakitekwa na tulilazimika kuweka polisi ili kuongeza usalama. …Serikali inaendelea kuimarisha usalama nchini,” alisema na kuongeza kuwa “Umuhimu wa jambo hilo (Mabasi kufanya kazi usiku na mchana) upo.”

Hata hivyo alisema, serikali inahitaji kujiridhisha kabla ya kuruhusu mabasi kufanya kazi usiku jambo ambalo amedai litawawezesha abiria kuwa na mipango binafsi ya kibiashara kutoka eneo moja kwenda jingine.

“Wito kwa watanzania kudumisha usalama,” alisema Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema amesha elekeza Mamlaka ya Serikali za Mitaa TAMISEMI kuhakikisha masoko makuu yanafanya kazi masaa 24.

Zoezi hilo, kwa mujibu wa Waziri Mkuu litaruhusu wale wanaokuwa “busy” ofisini kuweza kupata huduma wanapokuwa wametoka makazini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live