Menu ›
Biashara
Fri, 24 Mar 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja Serikali imejipanga kuboresha huduma kwa watalii katika nyanja mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi ikiwa ni mkakati wa kuwafanya watalii hao kuongeza siku za kukaa nchini na hatimaye kukuza pato la Taifa.
Amesema moja ya mkakati wa Serikali ni kuboresha huduma za malazi kwa watalii kwa kuzirejesha hoteli za wizara ambazo zinaendeshwa na sekta binafsi ambazo kwa ujumla wake hazifanyi vizuri.
Masanja amesema Serikali inaendelea mikakati ya kuhakikisha hoteli hizo mara baada kurejeshwa zinakuwa kinara kwa kutoa huduma bora kwa watalii.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live