Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kupitia upya tozo ya bandari

38c83bc7749eede21b67b08fd8034039.jpeg Serikali kupitia upya tozo ya bandari

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KUFUATIA kilio cha wananchi juu ya tozo, serikali imepanga kufanya kazi na wadau wa bandari kupitia upya tozo hizo.

Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Leonard Chamuriho ambapo alisema wanatarajia kufanya vikao na wananchi wa visiwa vya Yozu, Gembela na Soswa na Kasalazi, kwa lengo la kupokea maoni yao kabla ya kuidhinishwa kwa tozo mpya.

Kuali ya Dk Chamuriho imekuja kufuatia swali lililoulizwa na Mbunge wa Buchosa Erick Shigongo aliyetaka kujua ni lini serikali itaacha kutoza wananchi Shilinig 600 wakati wa kuingia na kutoka bandarini katika visiwa vya Kasalazi, Yozu, Gembela na Soswa kwa kisingizio cha uwekezaji?

Dk Chamuriho amesema, kiwango cha tozo ya abiria wanaopita katika bandari ndogo zilizopo katika maeneo mbalimbali ya mwambao wa bahari na maziwa, ni Shilinig 600.

“kama ambavyo imeainishwa katika kitabu cha tozo (tariff books) cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA). Hata hivyo, TPA baada ya kupokea malalamiko ya wadau mbalimbali kuhusu tozo hizo, imeanza kuchukua hatua za kufanya marejeo ya tozo hizo kwa bandari zote ndogo nchini,” amesema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz