Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuongeza uzalishaji wa sukari nchini

Sukarisssssssssss Serikali kuongeza uzalishaji wa sukari nchini

Sat, 2 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema kuwa imejipanga kuongeza uzalishaji wa sukari katika kiwanda cha Kilombero ili kuweza kupambana na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo katika soko la ndani.

Haya yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari Mkoani Morogoro, Oktoba 2,2021, na kubainisha kuwa Serikali ina jumla ya hisa asilimia 25 katika kiwanda hicho.

Msigwa amesema kuwa, upanuzi wa kiwanda hicho umelenga katika kuongeza uzalishaji kutoka Tani 130,000 hadi 260,000.

“Mradi mkubwa unafanyika wa upanuzi wa kile kiwanda tunataka kile kiwanda kiongeze uzalishaji wa sukari kutoka tani 130,000 hadi kufikia tani 260,000”

“Mbali na kukabiliana na upungufu wa Sukari ,tunataka kuzalisha sukari ya ziada ,tunataka tufike hadi tani 625,000 ifikapo mwaka 2025” amesema Msigwa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live