Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuondoa leseni za biashara halmashauri - VIDEO

Serikali Kuondoa Leseni Za Biashara Halmashauri Serikali kuondoa leseni za biashara halmashauri

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara nchini ambapo sasa wanaondoa leseni katika Halmashauri.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji alipokutana wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuwasikiliza pamoja na kutatua changamoto zinawazowakabili.

"Tulichokiamua tunataka kuwaambia ndugu zetu wa TAMISEMI kazi tuliyotaka muifanye sasa tutafanya wenyewe, unaingia kwenye simu yako unaoomba leseni BRELA unapewa leseni itakayokuwezesha kufanya biashara nchi nzima," alisema Dkt Kijaji.

Dk. Kijaji amesema kuwa tangu kuanza kutekelezwa kwa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara hapa nchini (Blue Print), Serikali imefanikiwa kuondoa kodi, tozo na ushuru mbalimbali 374 kati ya 380.

“Tulianza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara mwaka 2019 na tulitamani kuondoa kodi, tozo pamoja na ushuru mbalimbali zilizokuwa zikilalamikiwa na wafanyabiashara nchini ambazo zilikuwa 380 kwa miaka Mitano.

Lakini leo tuko mwaka wa Nne tunatekeleza na tumeshaondoa kodi, tozo na ushuru 374 zimebaki Sita tuu na Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuzimaliza changamoto hizi zote lengo likiwa ni kuhakikisha mnafanyabiashara katika mazingira mazuri na wawekezaji wanawekeza katika mazingira mazuri na yanayoibuka tunayabeba na kuendelea kushughulika nayo,” amesema Waziri Kijaji.

Dk. Kijaji pia ameagiza kitabu kinachoainisha kodi hizo zilizoondolewa kichapishwe ndani ya wiki moja na kifikishwe kwa Wakuu wa Mikoa ili wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali wajue kodi zipi zilizoondolewa kupunguza migogoro kati ya wafanyabishara na serikali.

View this post on Instagram

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live