Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kununua mahindi tani 10,400

842b8c7ecb149f7c7cc390502b815ed0 Mahindi

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imeielekeza Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) inunue mahindi tani 10,400 zilizohifadhiwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula-NFRA Kanda ya Makambako.

Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda alisema CPB imepewa jukumu la kununua na kuuza nafaka hivyo inapaswa kununua mahindi hayo.

Mkenda alisema hayo wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Njombe iliyoanza juzi.

Alisema mahindi hayo anapswa kuzungushwa/kuuzwa ili kutoa fursa kwa NFRA kuingia sokoni kununua mahindi mengine.

"NFRA ikiingia sokoni itatoa nafasi kwa wakulima watakaouza mahindi yao kuweza kununua pembejeo bora na kulima zaidi mazao ya nafaka" Amekaririwa Waziri Mkenda

Alisema kazi ya NFRA ni kununua nafaka na kuhifadhi ili ikitokea changamoto yoyote nchini nafaka hiyo iweze kutolewa lakini kwa kuwa hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza nchini kwa kipindi cha miaka mitatu hivyo wanapaswa kuyauza ili kununua mahindi mengine kwa ajili ya kuhifadhi.

Profesa Mkenda alisema pamoja na mahindi yaliyohifadhiwa kwenye ghala la NFRA Makambako lakini pia kuna tani 5,009.267 za mpunga ambazo pia zitafutiwe masoko hasa nje ya nchi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz