Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kumaliza changamoto ya malisho

Malisho Mifugo Ngombe Serikali kumaliza changamoto ya malisho

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema serikali inatafuta suluhu ya kudumu katika kuondoa changamoto ya uvamizi wa maeneo yote ya malisho, ili kusaidia wafugaji kufuga vizuri, huku wakiwa na uhakika wa chakula cha kutosha kwa mifugo yao.

Waziri Ulega ametoa kauli hiyo kijijini Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga, alipowatembelea wakazi wa eneo hilo ili kujionea shamba darasa la malisho lenye ukubwa wa hekari 20.

Amesema taratibu zitakazowekwa ni lazima zisimamiwe na mamlaka za wilaya na yeyote akatakayekiuka atachukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu wa wilaya ya Handeni Albert Msando amesema wakazi wa kijiji cha Msomera hawana tatizo lolote na serikali wala wizara hiyo, hivyo kuiomba jamii kupuuza yanayosemwa na baadhi ya watu wasioitakia mema serikali katika utekelezaji wa majukumu yake.

Amesema Kijiji cha Msomera ni kijiji kilichopangwa kwa kufuata mpango wa matumizi bora ya ardhi, ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo ya malisho na josho kwa ajili ya mifugo.

Kwa awamu ya kwanza mpaka sasa tayari kaya 500 zimeshaanza makazi mapya kijijini Msomera, zikitokea hifadhi ya taifa ya Ngorongoro na awamu ya pili ya kuwapokea wengine inatarajia kuanza wiki ijayo Septemba 25.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live