Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kula sahani na wafanyabiashara mtandaoni

Mtandao Biashara Serikali kula sahani na wafanyabiashara mtandaoni

Fri, 11 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imewataka watu wote wanaofanya biashara kidigitali kujisalimia kwenye ofisi za mamlaka hiyo ili wasajili biashara zao.

Taarifa iliyopatika kwenye mtandao wa Mamlaka hiyo inasema kuwa TRA itashirikiana na mataifa mbalimbali ya Afrika ili wananchi wote walipe kodi hasa wale wanaoendana na kasi ya teknolojia kwa kuwa ujenzi wa ujenzi wa taifa ni wa wote.

“Tunatambua kuna watu hawana maduka na hawana TIN kwa ajili ya biashara wanazofanya. Na wengine wana maghala makubwa ya kuhifadhi bidhaa na kisha kuuza kidigitali, sasa nyinyi nyote mnapaswa kuja kujisajili.” imesema taarifa hiyo na kuongeza

“Sambamba na hilo tunaendelea kufatilia wateja wenu mnaowahudumia ili tupate taarifa sahihi za biashara zenu.” imesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live