Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kula sahani moja na watorosha madini

Madini Ofii Geita Serikali kula sahani moja na watorosha madini

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini Dkt Dotto Biteko amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuhakikisha wanaendesha shughuli zao kwa kufuata sheria na kanuni za madini na kusisitiza kuwa Serikali haitamwonea huruma mtu yeyote ayakayebainika anatorosha madini.

Waziri Biteko ameyasema hayo leo Februari 21, 2022 wakati akikabidhi Tume ya Madini magari saba kati ya magari 40 yanayotarajiwa kutolewa na Serikali kama moja ya mikakati ya kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa maduhuli kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini.

Aidha mbali na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Waziri Biteko amesema kuwa magari hayo yatatumika kama kichocheo cha ukusanyaji wa maduhuli kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini.

Ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kununua vifaa vingine kama vile mashine za kupima madini kwenye masoko ya madini na kusimamia kwa karibu shughuli za madini ili kuhakikisha Serikali inapata mapato yake stahiki.

Aidha, amewataka watendaji wa Tume ya Madini kuhakikisha magari yanatunzwa na kuendelea kuchapa kazi kwa ubunifu mkubwa ili kuhakikisha lengo la kukusanya shilingi bilioni 650 kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 linafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

Katika hatua nyingine akizungumzia mikakati iliyowekwa na Wizara ya Madini kwenye udhibiti wa utoroshaji wa madini, Dkt. Biteko amesema kuwa mikakati iliyowekwa ni pamoja na kuongeza maafisa kwenye usimamizi wa shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula sambamba na kuishukuru Wizara ya Madini kwa ununuzi wa magari kwa ajili ya kutumiwa kwenye shughuli za madini amesema kuwa magari yatarahisisha kwa kiasi kikubwa utendaji kazi kwa kufika maeneo yasiyofikika kirahisi.

Wakati huohuo Waziri Biteko pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Ibrahimu Uwizeye wamezindua maonesho ya kimataifa ya madini yanayoendelea katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ikiwa ni sehemu ya mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini unaotarajiwa kuanza mapema kesho tarehe 22 Februari, 2022.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda kwenye maonesho hayo, Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Ibrahim Uwizeye amepongeza maandalizi na kufafanua kuwa nchi ya Burundi inaendelea kujifunza kuhusu usimamizi kwenye Sekta ya Madini Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live