Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kukomesha uvuvi haramu

Uvuvi Haramu Serikali kukomesha uvuvi haramu

Wed, 18 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema Serikali imejipanga kukomesha uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria.

Hayo ameyasema Mei 16, mwaka huu kwenye kikao cha Wadau wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa chenye lengo la kujadili changamoto za uvuvi kilichowakutanisha wavuvi, wachakataji wa mazao ya uvuvi,Watengenezaji na wasambazaji wa zana za uvuvi, wawakilishi wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba, wawakilishi wa usambazaji wa taa za sola, Watendaji wa Wizara.

Amesema kuendelea kwa uvuvi haramu kwenye ziwa Victoria kutasababisha kuwa janga ni vema kila mtu kulinda rasilimali za nchi kwa kufuata sheria kwa kuvua uvuvi halali.

“Mmekili uvuvi haramu umekithili mkiendelea kufanya hivyo samaki na dagaa wataisha na kutakuwa na janga kwani asilimia kubwa ya wananchi wanategemea ziwa victoria kwa kufanya uvuvi.

“Tunatakiwa tuulilinde ziwa letu ili tuendelee kufanya shughuli zetu za kujipatia kipato hivyo ni vema kila mtu anawajibu wa kubadilika kwanzia kichwani mpaka kwenye vitendo vyetu kwa kuvua uvuvi halali,” amesema Ndaki.

Amesema uvuvi haramu unaendelea hivi sasa unaanzia kwa mvuvi, msimamizi,viwandani Kwa sababu hawatoi taarifa pindi wanapoletewa samaki wadogo, kila mtu anawajibu wa kutoa taarifa ili kukomesha vitendo hivyo.

“Mtu wa kwanza anayeshiliki na uvuvi haramu ni mvuvi mwenyewe kwa sababu ndiye anakula kupitia hapo ni lazima kuwafichua wanaofanya vitendo hivi ili sheria ichukuliwe.

“Mkiendelea na uvuvi haramu tutatumia nguvu kukomesha vitendo hivi tusilaumiane maana tumepewa dhamana ya kulingana rasiliamali hizi ni lazima tuzilinde kwa hali na mali,” ameongeza Waziri Ndaki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live