Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kukifungua Kisiwa cha Pemba kiutalii

Serikali Kukifungua Kisiwa Cha Pemba Kiutalii Serikali kukifungua Kisiwa cha Pemba kiutalii

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamisheni ya Utalii Zanzibar inatarajia kufanya Bonanza la Utalii, Utamaduni na Michezo Kisiwani Pemba kaunzia tarehe 28/11/2023 mpaka tarehe 03/12/2023. Bonanza hilo linajulikana kama “Pemba Tourisport and Cultural Bonanza” (PTCB). Kwa mwaka 2023 ikiwa ni mkakati maalum wa kuifungua Pemba kiutalii

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Hafsa Mbamba ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari katika ofisi za wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Mbamba amesema Bonaza hilo ambazo litakuwa ni Bonanza la 4 kwa kufanyika katika kisiwa cha Pemba ambalo ni muhimu katika kuboresha kisiwa cha Pemba kwa kuwaunganisha wananchi pamoja na tamaduni zao, michezo, urithi na vivutio vya asili.

Aidha amesema dhamira ya serikali ni kuifungua Pemba kiutalii huku akitaja kuwa sekta ya Utalii hujachangia kwa asilimia 29.2% ya pato la taifa na inachangia kwa asilimia 80 ya upatikanaji wa fedha za kigeni kwa Zanzibar.

Miongoni mwa michezo itayokuweko katika bonaza hilo ni pamoja na mchezo wa Triathlon, kuongelea, kuendesha baiskeli na kukimbia pamoja na Mashindano ya Duffu, Mashindano ya Ngalawa, na mchezo wa Ng’ombe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live