Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kukifanya kilimo kuwa suluhisho la ajira

Kilimo Serikali kukifanya kilimo kuwa suluhisho la ajira

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: mwananchi.com

Mweli ameyasema hayo leo Juni 3 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mradi wa Farm Clinic ulioanzishwa na kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) kwa kushirikiana na kampuni ya Vodacom kwa lengo la kuwawezesha wakulima.

Amesema katika kutekeleza dhamira hiyo, Wizara ya Kilimo imepata eneo la hekta 7,000 mkoani Dodoma ambazo zitatumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na ardhi hiyo itagawiwa kwa vijana ili wafanye kilimo cha umwagiliaji.

Amesema vijana hao wakianza kilimo, wataanzisha vyama vya ushirika ili wajue wapi wanauza mazao yao moja kwa moja baada ya mavuno ya mazao yao.

"Wizara tutakuwa na kituo cha taarifa, yoyote ambaye ana suluhisho, tunamkaribisha, tuko open kwa yoyote mwenye mawazo bora ya kumwinua mkulima," amesema naibu katibu mkuu huyo.

Amebainisha kwamba baadhi ya mipango ya serikali mwaka huu katika sekta ya kilimo ni pamoja na kuimarisha tafiti ili kuhakikisha kwamba mbegu bora za kutosha zinapatikana hapa nchini na Tanzania unaacha kuagiza mafuta ya kula.

Mweli amesisitiza kwamba serikali inalenga kujitosheleza kwenye mahitaji ya chakula na kupunguza utegemezi wa chakula kutoka nje hasa uagizaji wa mafuta ya kula.

"Bado tunaagiza mafuta ya kula lakini mwaka huu tunakwenda kugawa mbegu za alizeti kwa wakulima. Tunatarajia mwakani tatizo hili litapungua kwa kiasi kikubwa," amesema kiongozi huyo aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Amesema mwaka huu serikali imetenga Sh150 bilioni kwa ajili ya kutoa ruzuku ya mbolea na pia watahakikisha kwamba wakulima wote wanasajiliwa ili wajue wanamsaidia nani.

Chanzo: mwananchi.com