Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kukarabati madaraja, barabara

Bashungwa Attached Miezi Miwili Kwa CRB Na NCC Kuunda Mabaraza Ya Wafanyakazi Serikali kukarabati madaraja, barabara

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amesema Serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) imejipanga kuhakikisha inarejesha mawasiliano ya barabara zote na madaraja yanayoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha ndani ya muda mfupi pindi yanapoharibiwa.

Aidha, Bashungwa amewaelekeza Mameneja wa TANROADS Mikoa yote kuendelea kufanya ukaguzi wa madaraja na makalavati pamoja na kuondoa matope na takataka ambapo ametaka zoezi hilo kuwa endelevu.

Bashungwa ametoa agizo hilo leo Mkuranga Mkoani Pwani wakati akikagua zoezi la urejeshaji wa miundombinu ya barabara kuu ya Pwani - Lindi katika eneo la Kimanzichana Kusini lililoathiriwa na mvua na kusababisha barabara hiyo kufungwa kwa muda.

Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Mohamed Besta, kusimamia kikamilifu Wakandarasi wote waliopewa kazi ya kurejesha miundombinu iliyoathiriwa na mvua kufanya kazi kwa ufanisi na kumaliza ndani ya wakati.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani, Eng. Baraka Mwambage amesema tayari wamepokea kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya matengenezo ya dharura ya miundombinu ya barabara na madaraja na timu ya wataalamu imejipanga katika maeneo mbalimbali kuendelea kurudisha mawasiliano yaliyopata athari za mvua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live