Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kujenga soko la madini Butiama

Vibali Madini (600 X 303) Serikali kujenga soko la madini Butiama

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Madini, Dk Stephen Kiruswa amesema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho kwaajili ya kuanza ujenzi wa soko la madini wilayani Butiama mkoani Mara.

Dk Kiruswa amesema kuwa serikali inatambua mchango unaotokana na sekta ya madini hivyo ni wajibu wake kuhakikisha kuwa mazingira yanakuwa mazuri.

"Tunataka muwe na soko zuri kama wenzenu wa sehemu zingine kama vile Geita na hii itaboresga na kurahisisha shughuli zenu amesema" Dk Kiruswa.

Naye Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa, Kupitia mradi wa maji wa Mugango- Kiabakari- Butiama utasaidia kumaliza changamoto ya maji katika wilaya ya Butiama.

Amesema mbali na mradi huo lakini wapo kwenye mchakato wa kufunga pampu katika mradi wa maji wa Butiama ambao umeshindwa kutoa maji kwa muda baada ya pambu hiyo kuharibika hivyo kukakimilika kwa ufungaji huo pia kutasaidia kuondoa tatizo la ukosefu wa maji katika mji wa Butiama

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Moses Kaegele ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa 72, na shule shikizi vyumba vyumba 6.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live