Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kujenga soko la kimataifa la nafaka Tanga

Waziri Bashe Serikali kujenga soko la kimataifa la nafaka Tanga

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (Mb) akiwa Mkoani Tanga leo Tarehe 12/12/2023 ambapo ameanza ziara yake ya siku tatu amesema Moja ya Mipango ya Serikali katika kurahisha bishara mipakani ni kujenga masoko katika Mipaka yetu na nchi jirani. Katika kuteleleza hilo Wizara ya kilimo kupitia bajeti ya mwaka 2023/2024 itajenga soko katika mpaka wa Horohoro Wilaya ya Mkinga litakalohudumia wafanyabishara katika mpaka huo.

Bashe ameleeza kuwa ni Mpango wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuimarisha biashara ya kimataifa ya mazao ya nafaka kwa nchi jirani, kwani kufanya hivyo kutalinda wakulima wadogo dhidi ya ulanguzi wa bei ya mazao; kurahisisha ukusanyaji wa tozo za Serikali; kuongeza mapato yatonayo na fedha za kigeni na kuwarahisishia wafanyabishara upatikanaji wa nafaka kirahisi.

Aidha wamekubaliana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya soko hilo na kilimo cha mashamba makubwa ya blockfarms ili kuzalisha kwa wingi na kutimiza adhma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya utekelezaji wa dira ya serikali ya kuilisha Afrika na Dunia kibiashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live