Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kujenga masoko ya kimkakati mipakani

Masoko Pic Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: Mwananchi

Wakulima nchini sasa wameondolewa hofu baada ya Serikali kuweka wazi azma yake ya kuendelea na majadiliano na nchi mbalimbali, lengo likiwa ni kutimiza mkakati wake wa kufungua masoko ya kimkakati ya mazao katika nchi hizo.

Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde ameyasema hayo leo Jumatano, Juni 21, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa Vitimaalum Stella Fiyao.

Mbunge huyo amehoji Serikali ina mkakati gani wa kutafuta masoko ya mazao ya kilimo.

Akijibu swali hilo, Mavunde amesema Serikali kupitia Wizara ya Kilimo itaendelea kuimarisha upatikanaji wa masoko ya mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi kwa kujenga masoko ya kimkakati mipakani.

Amesema pia Serikali inaimarisha kwa kujenga vituo vya masoko (market sheds) na kuboresha miundombinu ya maabara za Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viatilifu Tanzania (TPHPA) ili ziweze kupata ithibati itakayowezesha kufanya uchunguzi na kutoa vyeti vya ubora vinavyokubalika Kimataifa na kuongeza tija na kupunguza gharama za uzalishaji.

Aidha, amesema Serikali inaendelea na majadiliano na nchi mbalimbali na kufungua masoko ya mazao katika nchi hizo.

Amesema hadi sasa tumefanikiwa kufungua soko la Korosho nchini Marekani, soko la Parachichi China, India na Afrika Kusini na tunaendelea kuhudumia masoko ya nafaka katika nchi mbalimbali za Afrika.

Chanzo: Mwananchi