Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kujenga maghala vijijini

MAGHALA VIJIJINI Serikali kujenga maghala vijijini

Wed, 11 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde amesema serikali inakusudia kujenga maghala ya kuhifadhia mazao kuanzia ngazi ya kijiji.

Hatua hiyo inalenga kuwasaidia wakulima kuhifadhi mazao yao mara baada ya kuvuna, na kupunguza upotevu wa chakula mpaka kufikia chini ya asilimia 10 kufikia mwaka 2030.

Mavunde ameyasema hayo, wakati akizungumza na watumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, akiwa katika ziara yake ya siku moja Mkoani Katavi, baada ya kusomewa taarifa ya hali ya kilimo na changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo iliyowasilishwa na Mhandisi wa Kilimo Mkoa wa Katavi, Philipo Charles.

"Mazao mengi yanapotea na hiyo ni sehemu ya mapato yetu yanayopotea, lengo letu tuna tamani kuona Mtanzania kilimo chake kinamnufaisha," amesema Mavunde.

Amesema Mkoa wa Katavi ni moja kati ya mikoa ya kimkakati katika uzalishaji wa mazao, utakaochangia kuiongezea nchi thamani kwa uuzaji wa mazao nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live