Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kujenga chuo cha gesi Mtama?

Gesiii Serikali kujenga chuo cha gesi Mtama?

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema, Wananchi wa Mtama wametenga ardhi kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha gesi na kwamba wamekwishakabidhi eneo hilo kwa wizara ya Nishati wakisubiri maamuzi yafanyike kuhusu jambo hilo.

Waziri Nape ameyasema hayo alipokuwa akimkaribisha Rais Samia Suluhu Hassan kuzungumza na Wananchi waliokusanyika katika jimbo la Mtama wakati Rais Samia akiendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.

Amesisitiza kuwa Wananchi wa Mtama wanahitaji chuo hicho kujengwa katika eneo hilo kufuatia uwekezaji wa mradi wa gesi unaotarajiwa kutekelezwa siku zijazo ili kuweka uwiano wa mgawanyo wa maendeleo ndani ya mkoa wa Lindi kwani Lindi Mjini tayari vipo vyuo vingine.

Waziri Nape ameongeza kuwa faida za kujenga chuo cha gesi Mtama ni kwamba eneo hilo lipo katikati ya Lindi na Mtwara na zaidi ni kwamba Wananchi wa mikoa hiyo na ya jirani watapata fursa ya kujifunza namna ya kutoa huduma ya gesi na mafuta.

Aidha ameongeza kuwa matumaini ya mikoa hiyo miwili kujiimarisha kiuchumi yapo kwenye biashara ya gesi licha ya kuwa na zao la Korosho, Mbaazi na Ufuta kwa mikoa ya Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live