Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuja na mpango uchumi wa kidigitali

Uchumi Kidigitali.png Serikali kuja na mpango uchumi wa kidigitali

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga amesema kwa sasa serikali inapitia sera ya Taifa ya TEHAMA ya 2016 kwa lengo la kuja na sera itakayowezesha Tanzania kutengeneza mazingira mazuri kwa uchumi wa kidijitali.

Akizungumza wakati wa mdahalo kwenye kongamano la Afrika la usalama mitandaoni linalofanyika Kigali nchini Rwanda, Kipanga amesema

"Mpango huu wa kupitia sera ya Taifa ya TEHAMA unaenda sambamba na mpango kazi wa miaka kumi wa Tanzania kwenye uchumi wa kidijitali (Tanzania Digital Economy Strategic Framework 2023-2033) ambao ndio njia yetu kuelekea uchumi wa kidijitali"

Aidha Kipanga ameongeza kuwa, Serikali inaandaa utaratibu ambao utakuwa na utabulisho maalumu kwa watumiaji wa uchumi wa kidijitali

Chanzo: www.tanzaniaweb.live