Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuiongezea uwezo TIRDO

Viwanda Bubu Serikali kuiongezea uwezo TIRDO

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imekagua na kuridhishwa na Maendeleo ya ujenzi wa jengo la Utawala katika Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) ambalo linatarajiwa kumalizika June 30,2024.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi huo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deodatus Mwanyika amesema serikali imeongezea uwezo wa kimiundombinu TIRDO ambao walikuwa na majengo chakavu ambayo hayakuwa yanaenda na taasisi hiyo.

Aidha amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iridhihinisha jengo la utawala litengenezwe kwani jengo hilo lilisimama kwa muda mrefu.

Pamoja na hayo Kamati hiyo imeiomba serikali kupitia Wizara kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa kuleta bajeti iliyobakia.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema kwa hatua zilizobaki kukamilisha ujenzi wa jengo hilo, walikuwa na bajeti ya shilingi bilioni 3.4 ambapo mpaka sasa wameshapokea shilingi bilioni 1.54 kwaajili ya ukamilishani wa jengo hilo.

Waziri Kijaji ameishukuru Kamati hiyo kwa kuweza kuisukuma serikali na hatimae kupatikana kwa fedha hizo na ujenzi ukiendelea kutoka asilimia 50 iliyokuwepo mwaka jana na kufikia kwasasa asilimia 73.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live