Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuinua biashara ya dagaa wa Kigoma

Dagaa Kigoma Serikali kuinua biashara ya dagaa wa Kigoma

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Serikali kupitia Wizara hiyo imejipanga kuhakikisha Dagaa wa Kigoma wanakuwa ni zao la kimkakati kibiashara litakalokwenda kuvutia uwekezaji na kusisimua uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.

Ulega amesema hayo wakati akiongea na Wadau wa Uvuvi alipofanya kikao nao katika Mwalo wa Katonga uliopo Mkoani Kigoma mwishoni mwa wiki.

Amesema kuwa serikali imejipanga kufanya zao la dagaa wa Kigoma kuwa la kimkakati kwa sababu biashara ya dagaa inahusisha watu wengi katika jamii, hivyo kuiimarisha biashara hiyo ni kuwaimarisha wananchi kiuchumi.

"Sisi Serikali tunataka kuinua biashara ya dagaa wa Kigoma, tunataka wavuvi wainuke kiuchumi, na tumejipanga kuondoa vikwazo vyote vinavyowasumbua na tutalitangaza vyema zao hili ili kuvutia uwekezaji zaidi hapa Kigoma," amesema Ulega

Nao wadau wa biashara hiyo mkoani hapo wameiomba Serikali kuwasaidia wavuvi hao kuweza kupata nyavu zinazotakiwa ili waweze kuifanya shughuli hiyo kuwa ya kiuchumi ipasavyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live