Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuimarisha mazingira wezeshi kibiashara: Dkt. Mwinyi

334953676 952219752608886 7142464948404645728 N 1 1140x640 Serikali kuimarisha mazingira wezeshi kibiashara: Dkt. Mwinyi

Fri, 10 Mar 2023 Chanzo: Dar24

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema lengo la Serikali ni kuimarisha na kuweka mazingira mazuri wezeshi ya kibiashara katika uwekezaji nchini.

Rais Mwinyi ameyasema hayo hii leo Machi 10, 2023 wakati akizindua Muongozo wa Uwekezaji na Mfumo wa Kieletroniki wa Uwekezaji (ZIPA).

Mwongozo huo una madhumuni ya kurahisisha utoaji wa huduma kwa wawekezaji ikiwemo usajili na upatikanaji wa cheti cha uwekezaji wenye jina la”Zanzibar Investment Electronic Window” (ZieW).

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi pia amesema suala la kukuza uwekezaji ni moja ya malengo makuu ya Serikalina ya kuleta Maendeleo nchini.

Chanzo: Dar24