Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuifanyia mageuzi Tazara

TAZARA 1TAZARA Serikali kuifanyia mageuzi Tazara

Sat, 30 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ili kuongeza ufanisi katika usafirishaji mizigo kupitia reli, Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imesema inafanya jitihada kuboresha Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) kwa kuongeza uwezo wa idadi ya mizigo itakayosafirishwa na reli hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile alipofanya ziara kwenye ofisi kuu za Tazara na baadaye kwenda katika karakana za shirika hilo zizizopo jijini Dar es Salaam.

Kihenzile amesema malengo ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kubeba tani za mizigo zaidi ya milioni 30 na si kama ilivyo sasa ambapo shirika linasuasua.

“Tazara ilitengenezwa kwa ajili ya kubeba tani milioni tano, lakini bado tukaona haya siyo malengo kwa sababu kule Zambia na nchi zingine tuna mizigo ya zaidi ya tani milioni 10, japo hata tunapozungumza hapa hatujawahi kufikia hata tani milioni moja na laki tano mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1986 ndiyo tulibeba tani milioni moja na laki mbili.

“Kwa sasa tunazungumzia tani laki mbili hadi laki tatu na sitini kwa hiyo ukiangalia operation yetu bado iko chini kuliko hata ilivyokuwa Tazara ya zamani lakini maono ya Serikali sio haya,” amesema.

Kihenzile amesema kwa sasa wanatafuta mkandarasi wa kujenga bandari ya Bagamoyo itakayoongeza mizigo hata katika bandari za Mtwara na Dar es Salaam na maeneo mengine halafu kwa maono ya Tazara ya kubeba tani milioni tano ni jambo lisiloendana na malengo.

“Kwahiyo na huku lazima tuangalie namna ya kupanua ili tuendane na maono ya Serikali na wahakikishia Tazara itabeba mizigo zaidi ya tani milioni 30,” amesema na kuongeza...

“Kwa sasa tunafanya maboresho ya bandari zetu ambapo kwa pale Bagamoyo kutakuwa na meli kubwa zenye urefu wa mita 405 kisha tutaunganisha bandari hiyo na reli ili mizigo isafiri kwa njia hiyo. Kwa hiyo kupitia reli tutasafirisha mizigo mingi zaidi kwa haraka na salama,” amedadavua Kihenzile.

Pia amesetoa rai kwa shirika hilo kuendelea kusimamia mipango ya muda mfupi na mirefu ili kuhakikisha shirika linafanyiwa mageuzi. Amesema Serikali inajua na inafuatilia kwa jicho la karibu na inapanga mikakati ili kuunganisha nguvu na kinachokifirikiwa na wao ili walete mabadiliko.

“Tukiboresha tunaongeza ajira tunarahisisha shughuli za watu. Watu wetu wanalalamika wakiona shirika hili muhimu linashindwa kusafirisha mizigo yao. Wenzetu Zambia wanawahimiza wafanyabiashari wasafirishe mizigo yao kupitia reli na sisi ndiyo wapokeaji na fursa hii ni yetu,” amesema.

Vilevile amesema shirika bado linajiendesha kwa namna ya kusua sua pamoja na hayo amesema waendeni wakayafanyie kazi wawe wabunifu ili shirika lijiendeshe kwa faida kwa sababu serikali inawekeza pesa nyingi.

“Na muendelee kuweka mikakati inayotekelezeka katika kulinda miundombinu dhidi ya hujuma.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tazara, Mhandisi Bruno Ching’andu amesema wameyapokea maelekezo ya Serikali na kuahidi kuyafanyia kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live