Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuifanya Coco Beach kuwa eneo la utalii wa ndani

5493fd534f4845a5b356122d57a979b6 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala, amesema serikali ina mpango wa kuboresha fukwe za bahari zilizopo katika mkoa huo kwaajili ya utalii na biashara.

Akizungumza jana wakati wa ziara yake katika Ufukwe wa Coco beach uliopo Wilaya ya Kinondoni, Makala, amesema hatua ya uboreshaji huo utafanya maeneo hayo kuwavutia watu wengi na kupenda kupatembelea.

"Kuna changamoto ya kutumia eneo la Coco beach vizuri na serikali sasa inaendeleza maeneo hayo ili yawe ya kitalii na tunaboresha mazingira ili wananchi wapate kupumzika hivyo zinatakiwa kuwa safi.

"Rais Samia na Makamu wa rais walinipa maelekezo hivyo uboreshaji utafanyika hatua kwa hatua kunazia ufukwe wa Ocean Road,kigamboni,Ilala hadi Coco,"alisema.

Amesema wamefanya mazungumzo na wadau mbalimbali ili kuleta boti za kuogelea na kuweka vibanda vinavyofanana vya wafanyabishara.

"Tutafanya Coco beach pati ambapo wasanii tofautitofauti watafanya show zao na tutaalika watu jiji zima,vyoo vitajengwa na maeneo ya miamala watakuwepo.

Amesema wafanyabishara wote walioko eneo la Cocobeach wapo kihalali hivyo wanatakiwa kuorodhesha majina yao ili kuwekewa mazingira mazuri.

"Na pia nyie ni wadau mnatakiwa kuzingatia usafi katika maeneo yenu hatutaki kuwa na ufukwe ambao ukiingia unashika pua.

Aliwataka wafanyabishara wa eneo hilo kujiunga katika makundi ili kupata mkopo wa asilimia 10 kutoka halmashauri.

Makala amesema mkakati mwingine ni kuweka umeme katika maeneo hayo huku akimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kufanya utaratibu huo.

"Lakini pia nataka vyombo vya usalama kuwa macho kwani nawatahadharisha wale vibaka wanaukuja kuiba mwisho wao umefika.

Aliwaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote za jiji kufanya ukarabati wa barabara zote ndani ya jiji.

"Lakini kingine maeneo yote ambayo hayaruhusiwi kufanya biashara mabango yawekwe sio kila sehemu watu wanafanya tu biashara.

Mmoja wa wafanyabishara katika eneo hilo Salum Abdallah alisema hatua ya serikali ni neema kwao na wanasubiria kwa hamu uboreshaji huo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz