Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya nyama

Ea139fe321e62c75763f49c762f1971a Serikali kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya nyama

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema, Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuhamasisha uwekezajii zaidi katika viwanda vya kuchakata na kusindika nyama kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi hususani nchi za Mashariki ya Kati.

Amesema kuongezeka kwa viwanda na machinjio zinazoweza kuuza nyama nje ya nchi, kwa sasa kuna machinjio na viwanda 24 vinavyokidhi vigezo vya kuuza nyama nje ya nchi ambapo vitanokati ya hivyo vimeanza kufanya mauzo nje ya nchi.

Pia, soko la nje ya nchi limeendelea kupanuka ambapo kwa sasa Tanzania inaweza kuuza nyama nchi za Omani, Kuwait, Bahrain, Saudi Arabia, Quatar, Honkong, Vietnam na Comoro. Jitihada hizi zimesaidia kuongezeka kwa kiasi cha nyama kinachouzwa nje ya nchi pamoja na mapato ya fedha za kigeni.

"Kutokana na marekebisho ya tozo za kuuza nyama nje ya nchi na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan za kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali duniani, biashara ya nyama nje ya nchi imeendelea kukua. Kwa mfano, kwa kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Januari 2022, Tanzania imeuza nje ya nchi jumla ya tani 5,362.9 zenye thamani ya dola za kimarekani 22,442,111.96, mauzo hayo ni sawa na ongezeko la asilimia 202 kwa kipindi cha miezi saba ya mwaka wa fedha wa 2021/22 ikilinganishwa na tani 1,774.29 zenye thamani ya dola za Kimarekani 4,290,000 zilizouzwa nje ya nchi katika kipindi cha mwaka mzima wa fedha wa 2020/21.

Amesema serikali ya awamu ya sita inaendelea kuboresha mazingira ya biashara, kuvutia uwekezaji mpya pamoja na majadiliano ya kibiashara na wadau kutoka nchi mbalimbali ili kufunguka masoko mapya ya nyama. Kutokana na jitihada hizo Tanzania na Saudi Arabia zimekubaliana katika biashara ya nyama, ambapo Tanzania itakuwa inapeleka nyama katika soko la Saudi Arabia.

Amesema soko la Saudi Arabia linakadiriwa kuwa na mahitaji ya tani 700,000 za nyama kwa mwaka, hivyo viwanda vya nyama hapa nchi vitaongeza uzalishaji hali itakayoongeza soko la mifugo kutoka kwa wafugaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live