Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kufungua maghala ya mazao ya chakula Kenya, DR Congo

20ffe21b28e2e0773476edfe25de582f Serikali kufungua maghala ya mazao ya chakula Kenya, DR Congo

Sat, 20 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imeanza majadiliano kufungua maghala makubwa mawili ya chakula nchini Kenya na jingine mjini Lubumbashi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kuongeza wigo wa masoko ya mazao hayo katika nchi hizo.

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema katika Mjadala wa Kitaifa kuhusu mchango wa Diplomasia ya Uchumi na Mahusiano ya Kimataifa katika kuchochea fursa za maendeleoq kwa wananchi kupitia sekta ya kilimo kuwa tayari Tanzania imekwesha fungua ghala kubwa nchini Sudan Kusini.

Kwa mujibu wa Bashe diplomasia ya kiuchumi ni kichocheo muhimu katika kufungua masoko hasa ya mazao ya kilimo yanazo zalishwa kwa wingi nchini.

Tanzania imekuwa ikizalisha chakula kwa wingi hata hivyo imeendelea kupata changamoto katika kuyafikia masoko tarajiwa. Kwa msimu wa kilimo, 2020/21 Tanzani ilipata chakula cha ziada cha zaidi ya tani milioni 3.3. Kwa upande mwingine Kenya, hutumia zaidi ya asilimia 50 ya kipato chake kwenye chakula.

“Utashangaa kuwa kabla ya mazungumzo kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Tanzania haikuweza kuuza chakula cha kutosha Kenya,” amesema.

Kitakwimu, Hadi mwezi Machi, Tanzania ilikuwa imepeleza tani 4,372 tu. Lakini baada ya mazungumzo kuondoa vikwazo visivyo vya kikodi, Tanzania ilipeleka zaidi ya tani 30,900 mwezi Juni na tani 54,000 mwezi Julai.

Amesema serikali haina shamba hivyo imejidhatiti kwenye kujenga miundombinu wezeshi na kwamba kama kujenga maghala na kununua mazao ili kuchechemua bei ya soko la ndani. Hata hivyo baadhi ya wakulima na wafanya biashara waliokuwa wakiuza mazao Sudan Kusini walilazimika kupita Uganda na badaye kuwa na madalili hivyo kuendelea kumgandamiza mkulima.

“Kuanzia sasa tumeamua kudevelop infrastructure (kutengeneza miundombinu) katika nchi tunazo tambua kuna masoko. Tunavyoongoa sasa tumefungua ghala kubwa Sudan Kusini, litatumiwa na serikali na Sekta Binafsi,” amesema Bashe na kusisitiza kuwa ghala hilo pia litakuwa na kituo kikubwa cha maonesho na mauzo.

Akifafanua, Naibu Waziri Bashe amesema jitihada za serikali ni kufungua ghala moja Mombasa na jingine Nairobi. Amesema anakusudia kutembelea nchi ya Zambia kutafuta suluhu ya vikwazo visivyo vya kikodi ili kuwezesha wafanyabiashara kulifikua soko la Lubumbashi kupitia Zambia.

Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda amekwisa zuru Burundi na kwamba majadiliano yanaendelea kufikia soko la Rwanda ili Tanzania iweze kuhudumi ukanda wote wa kaskazini.

Kuhusu ubora wa mazao ya chakula, serikali imesema imekwisha andaa utaratibu ikiwa ni pamoja na kuwezesha kuanzishwa kwa maabara zinazotambulika kimataifa kupima ubora wa mazao hayo. Vilevile Serikali imeanzisha mamlaka mahususi kusimamia mazao.

Chanzo: www.habarileo.co.tz