Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kufufua viwanda vilivyokufa

D2850799759aa97a174e1efd31cd333d Mwarobaini viwanda vilivyokufa wapatikana

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema mkakati wa serikali ni kuhakikisha changamoto zinazovikabili viwanda vilivyokufa zinatatuliwa ili viweze kufanyakazi.

Alisema hayo bungeni jana wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kawe, Askofu Gwajima (CCM) lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge mwenzake, Deo Mwanyika.

Katika swali lake, Gwajima alitaka kujua mkakati wa serikali kuwasaidia wenye viwanda vilivyokufa au havifanyikazi kwa sababu mbalimbali kikiwamo kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Famili kilichopo Salasala, Jimbo la Kawe.

Kigahe alisema mkakati wa serikali kupitia utekelezaji wa Blue Print ni kuhakikisha changamoto zote zinazovikabili viwanda zinatatuliwa ili kuviwezesha kufanyakazi ikiwamo kiwanda cha mafuta cha Familia.

Naye, Mbunge wa Kilwa Kusini, Ally Kassinge alitaka kujua hatua iliyofikiwa katika mazungumzo kati ya serikali na wawekezaji kwa ajili ya kujenga kiwanda cha mbolea kutokana na gesi asilia.

Akijibu, Kigahe alisema azma ya serikali ni kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa mbolea. “Mahitaji ya mbolea nchini ni tani 700,000, lakini uwezo wa nchi katika kuzalisha mbolea haufiki tani 100,000. Lengo la serikali ni kutumia gesi asilia kuongeza uzalishaji wa mbolea nchini,” alisema.

Katika swali la nyongeza la Mbunge wa Nachingwea, Amandus Chinguile alitaka kujua mkakati wa serikali wa kufufua viwanda viwili vya kupangua korosho na cha kuzalisha mafuta.

Kigahe alisema serikali ilifanya ubinafsishaji wa viwanda 156 na tathmini iliyofanywa mwaka 2017 ilibaini 88 vilikuwa vinafanyakazi na 68 vilikuwa havifanyikazi vizuri.

Alisema serikali imefanya kazi ya kuvirudisha viwanda 20 vikiwamo vya kuzalisha mafuta na kubangua korosho vya Nachingwea.

“Kuna viwanda tumeviweka kwenye eneo huru la uwekezaji na serikali inatafuta uwekezaji ili viweze kuzalisha mafuta na kubangua korosho kwa ajili ya mauzo ya nje,” alise

Chanzo: www.tanzaniaweb.live