Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kufanyia kazi mapendekezo sekta ya madini

Mikataba Ya Bandari Itazingatia Maslahi Ya Nchi   Majaliwa.jpeg Serikali kufanyia kazi mapendekezo sekta ya madini

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia wadau wa sekta ya madini kuwa Serikali itazingatia ushauri na mapendekezo yote yaliyotolewa katika jukwaa la uwekezaji la sekta ya madini Tanzania lililohitimishwa leo.

Akizungumza wakati akifunga jukwaa hilo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Majaliwa amesema mapendekezo na ushauri uliowasilishwa katika jukwaa hilo utazingatiwa ili kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye sekta ya madini nchini.

Majaliwa amewahamasisha wadau hao kuungana na taasisi za sekta ya madini nchini kuendeleza miradi iliyopo nchini na ile itakayoanzishwa kwa kuzingatia utaratibu utakaonufaisha pande zote mbili [mwekezaji na Serikali]

Aidha, amesema amefurahishwa kusikia kuwa maazimio ya mkutano uliofanyika mwaka jana yametekelezwa vizuri, moja ya maazimio hayo ilikuwa ni kutatua changamoto za mikopo kwa wachimbaji wadogo ambapo imeanzishwa benki ya wachimbaji hao kwa lengo la kuwapatia mikopo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live