Serikali imekiri kuwepo kwa tozo mbalimbali kwenye mazao yanayouzwa kwa mfumo wa ushirika kama pamba, korosho ambayo yanasababisha kuporomoka kwa bei.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kusimamia kwa ukaribu kuhakikisha wakulima wananufaika na mazao haya kwa kuwatafutia masoko na kuweka utaratibu mzuri wa tozo na ameagiza bodi za mazao hayo kufuatilia kwa ukaribu tozo zisiwe nyingi, ili kuona wanunuzi na wakulima wananufaika.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe leo Februari 8, 2024 kwenye Mkutano wa Kumi na Nne wa Bunge mjini Dodoma.