Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuboresha sekta ya anga

ATCL ATC Serikali kuboresha sekta ya anga

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeahidi kuendelea kuboresha sekta ya anga nchini kwa kutenga fedha kwa ajili ya kujenga na kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege, ununuzi wa rada pamoja na ununuzi wa ndege mpya.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa Jijini Dar es Salaam wakati akijibu hoja za Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Serikali iliyotengewa fedha kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo taasisi za TCAA, TAA, ATCL na KADCO ziliielezea kamati utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kisekta na maendeleo ya sekta ya usafirishaji kwa njia ya anga nchini.

Waziri Mbarawa amesema kuwa kupitia maelekezo ya Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa zile taasisi ambazo zina uwezo wa kuzalisha na kuajiri ziajiri moja kwa moja itasaidia sana kupunguza tatizo la uhaba wa watumishi katika taasisi hizo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Selemani Kakoso amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na utekelezaji na usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na mamlaka za usafiri wa anga Nchini ikiwemo zile za udhibiti, Uangalizi, Watumiaji na Waandaaji wa miundombinu ya usafiri wa Anga Nchini licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali

Chanzo: www.tanzaniaweb.live