SERIKALI imejipanga kuendelea kuboresha sekta ya kilimo kuelekea msimu mpya kwa kutoa ruzuku ya pembejeo kwa mazao yote tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita, lengo likiwa ni kuwapunguzia changamoto wakulima. - Pia imesema hadi sasa mbolea ya kupandia imeanza kuwasili nchini na inatarajiwa kufikia Agosti 15 mwaka huu, masoko yataanza kufunguliwa maeneo mbalimbali, ili kuhakikisha wakulima wanapata kwa wakati na kuwapunguzia usumbufu kama ilivyokuwa msimu uliopita. - Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe Julai 30,2023 akiwasilisha taarifa yake kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana, katika kikao cha ndani cha viongozi wa CCM Mkoa Tabora. - Amesema serikali inafahamu mwaka huu wakulima wa tumbaku hawakufurahia ruzuku,lakini msimu ujao ruzuku itakuwepo. - "Watu wote wapata ruzuku kama inavyostahili wote mtapata na kuanzia msimu huu wa kulimo, ruzuku tutaipeleka katika mazao yote ya kilimo na niwape taarifa mbolea ya kupandia tayari zimeshakuja," amesema Bashe.