Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuanzisha mfuko wa kinga-bei

Uchumi Kupanda Serikali kuanzisha mfuko wa kinga-bei

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa kutambua athari ya mabadiliko ya bei kwa wakulima wa pamba nchini, Serikali ipo katika hatua za awali za uanzishaji wa Mfuko wa Kinga ya Bei (Price Stabilization Fund) utakaotumika kumfidia mkulima wakati bei inaposhuka kwa kiasi kitakachokubalika kwa mujibu wa Sheria ya kuanzishwa kwake.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Stanslaus Nyongo wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo Mbunge huyo alitaka kujua lini Serikali itaanza kununua Pamba toka kwa wakulima pindi bei ya Pamba inapoporomoka katika soko la Dunia.

Silinde amesema kuwa kutokana na kutokuwiana kati ya uzalishaji na mahitaji ya pamba duniani, bei ya pamba hupanda na kushuka kulingana na hali ya wakati huo.

“Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita bei ya pamba kwa ratili katika soko la dunia mwaka 2020 ilifikia Senti 50 za Dola ya Marekani na mwaka 2021, bei ilipanda hadi kufikia Dola 1.5 kwa ratili. Mwaka 2023 hadi mwanzoni mwa 2024 bei ilikuwa wastani wa Senti 84.” Amesema Naibu Waziri Silinde.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live