Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15,2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba Serikali imekamilisha taratibu za kununua dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuanzisha akiba ya dhahabu hapa nchini.
“Kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa viwanda vya kusafishia dhahabu, Serikali itaendelea kuweka vivutio kwa viwanda hivyo ili vipate malighafi ya kutosha na ili kukamilisha hilo Serikali imepunguza mrahaba wa madini yanayouzwa kwenye viwanda hivyo kutoka 6% hadi 4%”
“Nafurahi kulijulisha Bunge kuwa Serikali imekamilisha taratibu za kununua dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuanzisha akiba ya dhahabu hapa nchini”
“Tunataka tunapotaja akiba ta fedha za kigeni tutaje na akiba ya dhahabu tuliyonayo, hatua hii itawapatia Wachimbaji bei nzuri na kuimarisha sarafu ya Nchi yetu, hii ni baada ya kupokea maelekezo ya Mh.Dkt. Samia na michango ya Waheshimiwa Wabunge”