Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuandaa mazingira rafiki uwekezaji wa viwanda

2ef98cf5a93b3fdd737a2e2c23669d9b Serikali kuandaa mazingira rafiki uwekezaji wa viwanda

Wed, 10 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kuvutia sekta binafsi kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vipya vya kubangua Korosho pamoja na kufufua vile vilivyopo.

Kigahe amebainisha hayo leo bungeni Jijini Dodoma alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Tunza Malapo lililojikita kufahamu ni lini Serikali itafufua viwanda vya kubangua Korosho vilivyopo katika Manispaa ya Mtwara Mkindani.

“Kabla ya zoezi la ubinafsishaji Serikali ilikuwa na viwanda 12 vya kubangua Korosho hapa nchini na viwili kati ya hivyo vilikuwa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani ambavyo vyote hadi hivi sasa vinaendelea kufanya kazi” amesema Kigahe.

Kigahe amebainisha kuwa viwanda hivyo vinaendelea na shughuli ya kubangua Korosho pamoja na kutoa huduma ya kupanga madaraja na kufungasha bidhaa hiyo kutoka kwa wakulima wadogo.

Chanzo: habarileo.co.tz