Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuwekeza kwenye vyanzo mbalimbali kwa ajili ya uzalishaji wa Nishati na Gesi asilia ili kuhakikisha Watanzania wananufaika na Uwepo wa Nishati hiyo ikiwemo ile Mbadala.
Waziri Mkuu Kassima Majaliwa ametoa kauli hiyo katika Mkutano mkuu wa 7 wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) unaoendelea mkoani Lindi.
"Niwahakikishie tu kama kuna wawekezaji kwenye eneo hili la Miradi ya Gesi, tutaendelea kuipokea miradi hii na kuijenga hapa nchini ilu tupate umeme wa Kutosha na Uhakika" amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mkoa wa Lindi umekuwa ukitekeleza miradi mbali mbali ya Gesi asilia, ambapo kukamilika kwake kutaisaidia Tanzania kuwa na kiwango kikubwa cha Nishati hiyo.