Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali imeridhishwa na makampuni ya utoaji huduma za mafuta na gesi nchini

Serikali Imeridhishwa Na Makampuni Ya Utoaji Huduma Za Mafuta Na Gesi Nchini Serikali imeridhishwa na makampuni ya utoaji huduma za mafuta na gesi nchini

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: millardayo

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga, amesema Serikali imeridhishwa na mwenendo wa kampuni hiyo katika utoajia wa huduma za mafuta, gesi na vilainishi na kuahidi kuendelea kuwa nayo bega kwa bega.

Naibu Waziri Judith ameipongeza kampuni hiyo kwa ubunifu mbalimbali inaoufanya ikiwemo kuwatambua na kutoa zawadi kwa waendeshaji bora wa vituo vya mafuta vilivyo chini ya kampuni hiyo nchi nzima ambao wanafanya vizuri zaidi katika maeneo mbalimbali ya utoaji wa huduma na bidhaa za Puma Energy.

Amesema huduma bora ndizo zinazoifanya kampuni hiyo iendelee kuwa namba moja kwa utoaji wa huduma za mafuta nchini, hivyo itaendelea kuiunga mkono kuhakikisha inaendelea kuwa katika ubora unaitakiwa na kuiletea nchi mapato zaidi.

Naibu Waziri Judith amesema kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Puma Energy Tanzani ni kiongozi wa soko katika usambazaji na uuzaji wa bidhaa za mafuta ya petrol nchini.

Akizungumza katika hafla ya kuwatangaza na kuwapa tuzo za watoa huduma bora wa Puma kwa mwaka 2023, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Fatma Abdallah amesema mafanikio makubwa inayoyapata Puma yanatokana weledi, kujituma na uwajibukaji unaofanyika vituoni.

Amesema watoa huduma hao wamekuwa wakiwapatia wateja wao huduma iliyobora kila wanapotembela vituoni, hivyo watoa huduma hao ndilo jicho la kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa Fatma lengo la kampuni hiyo ni kuwapa huduma bora Watanzania kufikia malengo yao katika maisha hivyo wataendelea kuboresha huduma kulingana na wakati na mahitaji.

Katika tuzo hizo Kituo cha Mafuta Cha Puma Arusha kiliibuka mshindi wa kwanza huku Puma Upanga ikitwaa nafasi pili kwa huduma bora.

Chanzo: millardayo