Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali imepoteza Tsh. Bilioni 22 biashara ya miti Sao Hill

USAFIRISHAJI Magogo UVIKO -19 yasababisha hasara ya milioni 22

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhifadhi mkuu wa shamba la miti la Sao Hill, Lucas Sabida amesema serikali imepata hasara ya shilingi bilioni 22 inayotokana na shamba la misitu la Sao Hill kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO-19.

Sabida amesema kuwa mwaka jana shamba hilo halikufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kutokana na kushuka kwa uchumi kutokana na kudorora kwa soko la mbao kutokana na mlipuko wa ugonjwa UVIKO 19.

“Kwa mwaka 2021 Wavunaji 323 Waliizinishwa kuvuna Hadi June 30 waliofanikiwa kuvuna ni 123,wengi wao walishindwa kuvuna kutokana na changamoto mbalimbali hivyo Uvunaji ulfikia asilimia 60 tu mapato ya serika bil 33.5 badala ya 55.5 sawa na hasara ya bilioni 22 changamoto kubwa ni kudorora kwa soko kutokana na Covid 19” alisema Sabida

Wananchi na wadau wa misitu wilayani Mufindi wametakiwa kuendelea kulilinda shamba la miti la Sao Hill kwa kuwa linachangia kwa asilimia kubwa uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Wadau wa uvunaji wa miti 368 katika shamba hilo wamesema kuwa shamba hilo limekuwa linasaidia kukuza uchumi wa wananchi kupitia malighafi za miti ambao zinapatikana hapo.

Mhifadhi mkuu wa shamba la miti la Sao Hill,Lucas Sabida amesema kuwa serikali itasimama kuhakikisha shamba hilo linakuwa chombo muhimu katika kutengeneza Ajira na ukuaji wa uchumi wa Wana Mufindi na Taifa kwa ujumla kwa kutegemea malighafi zote ambazo zinapatikana katika shamba hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live