Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali iliangalie kwa makini suala la mfumuko bei za vyakula-Musukuma

Maxresdefault 671x640.jpeg Serikali iliangalie kwa makini suala la mfumuko bei za vyakula-Musukuma

Sun, 5 Feb 2023 Chanzo: dar24

Mbunge wa Geita Vijijini Dkt.Joseph Kasheku Musukuma, amesema mfumuko wa bei unaitesa sana Tanzania kutokana na bidhaa mbalimbali kuuzwa kwa bei ghali ukiwemo mchele.

Dkt.Musukuma ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha uliopo Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.

Amesema ni vyema Serikali iliangalie suala hilo kwa jicho la tatu ili wananchi waweze kupata unafuu wa maisha kwa kununua vyakula kwa bei nafuu.

Aidha Musukuma, ameiomba Serikali ihamishe Shule ya Msingi Sahara iliyopo Wilaya ya Nyamagana ili wajenge machinga Complex ambayo itawaweka Wafanyabiashara hao pamoja hatua itakayosaidia kuondokana na changamoto ya kwenda nje ya mji ambayo inapelekea kufilisika kwa mitaji yao.

“Hakuna kitu kinaniumiza kichwa kama kuwaondoa wamachinga mjini suala la machinga limekuwa gumu hapa Mwanza ndio maana nimeamua kutoa mawazo yangu kwa kumuomba Rais wa Jamuhri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu kutenga eneo hilo la Shule ili machinga waweze kufanya biashara zao katika maeneo ya mjini”, amesema Dkt.Musukuma.

Chanzo: dar24