Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali bega kwa bega na SINO TAN

SINO TAN  SHEMDOE Katibu Mkuu wa TAMISEMI Profesa Riziki Shemdoe

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi mbalimbali wa Serikali wametembelea eneo la uwekezaji Kongani ya Viwanda 200 Kwala Kibaha Mkoani Pwani ambavyo vinajengwa na SINO TAN Industrial Park na kukutana na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Jansen Huang ambaye ameonesha michoro ya jinsi itakavyokuwa.

Katibu Mkuu wa TAMISEMI Profesa Riziki Shemdoe amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mama Samia Suluhu Hassan inampango mzuri wa kuindelezea Kwala sio tu kuwa eneo la kibiashara na uzalishaji lakini pia kuwa eneo la utalii Watu mbalimbali wakilitembelea kujionea mapinduzi yaliyofanywa

"Tuko hapa ambapo wenzetu wa SINO TAN wameshaanza kazi eneo hili na wanao mpango wa kutuonesha jinsi wanavyotaka kufanya kazi hii, na Serikali ya awamu ya sita ipo tayari kwa ajili ya kuenendeleza pamoja na kushirikiana na wenzetunhawa" Amesema Shemdoe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live