Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali: Zingatieni sheria ya vipimo

Mzani Wa Umeme Serikali: Zingatieni sheria ya vipimo

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Mbeya, Abogastin Kajungu amesema bado wananchi wengi mkoani humo hawatii sheria inayozuia vipimo vilivyopigwa marufuku kutumika kwa ajili ya kuuzia na kununulia bidhaa.

Kajungu ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kufanya ukaguzi wa vipimo katika kiwanda cha kuchakata mbegu bora za mazao ya kilimo cha Meru na kujiridhisha na usahihi wa vipimo vinavyotumika katika kiwanda hicho.

Amesema wananchi wengi mkoani Mbeya bado wanatumia vipimo ambavyo vimezuiwa yakiwemo magunia makubwa (lumbesa), madebe, na vifungashio visivyoruhusiwa na sheria iliyoanzisha Wakala wa Vipimo nchini.

Kwa upande wake, Meneja wa Kampuni ya Meru, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inayomiliki kiwanda cha kuchakata mbegu za mazao ya mahindi na maharage, amepongeza Wakala wa Vipimo kutoa elimu kwenye kampuni yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live