Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali Tanzania yajivunia akiba ya fedha za kigeni

49818 Pic+kigeni

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema inayo akiba ya fedha za kigeni ya kutosha na kwamba hadi Machi 30, 2019 ilikuwa na dola za Marekani 4.67 bilioni (sawa na zaidi ya Sh10 trilioni)

Akizungumza leo Jumatatu Aprili Mosi, katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema kiasi hicho cha fedha kina uwezo wa kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi kisichopungua miezi 4.8.

“Hivyo wasiwasi kuwa Serikali imechukua hatua ya kufunga baadhi ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni kwa sababu haina akiba ya fedha za kigeni si kweli hata kidogo,” amesema.

Amesema hofu kwamba nchi inarejea katika kipindi cha nyuma ambapo fedha za kigeni zilikuwa zinatolewa kwa vibali (rationing) ili kukidhi mahitaji ya fedha hizo kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo nazo hazina msingi.



Chanzo: mwananchi.co.tz